Alhamisi , 27th Mar , 2014

Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa viongozi wa shirikisho la michezo la serikali za mitaa Tanzania SHIMISEMITA uchaguzi uutakaofanyika kesho ijumaa march 28 mwaka huu jijini Tanga yamekamilika

Afisa michezo wa baraza la michezo Tanzania BMT Richard Mganga ambao ndio watasimamia zoezi hilo la uchaguzi amesema kuwa kila kitu ama taratibu zote zimekamilika likiwemo suala la usaili ambao umefanyika hii leo

Aidha Mganga amewakumbusha wajumbe na kuwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanakuja na viambatanisho vyote ambavyo vitawawezesha kuwa na sifa ya kupiga kura hapo kesho.