
Kocha wa tenisi walemavu Riziki Salum amesema, wapo katika maandilizi ya mashindano yatakayofanyika mwishoni mwa mwaka na mwakani lakini vifaa walivyo navyo ni chakavu ambapo vinachangia wachezaji kushindwa kucheza kwa bidii kutokana na uchakavu wa vifaa hivyo ikiwemo baskeli za walemavu ambazo huwasaidia katika mchezo huo.
Riziki amesema, wachezaji wanajituma katika mazoezi na wanafanya vizuri katika mashindano mbalimbali lakini vifaa ndio vinawaangusha huvyo serikali na jamii inatakiwa kujitokeza kusaidia ili hata timu ikifanya vizuri iwe ni manufaa kwa Tanzania kwa ujumla.