
Balozi Roeland van de Geer kushoto na Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dk.Augustine Mahiga.
Ufafanuzi wa taarifa hiyo umetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk.Augustine Mahiga ambapo ameweka wazi kuwa balozi huyo hajafukuzwa kama inavyoelezwa bali ameitwa makao makuu ya umoja huo.
''Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania, Roeland van de Geer anayetarajia kuondoka leo usiku kwenda makao makuu ya EU hajafukuzwa bali ameitwa na umoja huo kikazi'', imeeleza taarifa ya Waziri Dr.Mahiga.
Taarifa za kufukuzwa kwa balozi Roeland van de Geer zilisambaa usiku wa jana mitandaoni na kuzua mijadala mbalimbali hivyo ufafanuzi huu wa Waziri Mahiga umeondoa utata wote.
Hata hivyo Waziri Mahiga hajafafanua ni muda gani balozi atakuwa jijini Brussels, Ubelgiji ambako ndipo yalipo makao makuu ya umoja huo.