Jumatano , 21st Sep , 2022

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amewaongoza Wadau mbalimbali wa michezo katika hafla ya kuwaaga na kuwakabidhi bima za Afya kikosi cha Serengeti Girls kinachokwenda kushiriki fainali za kombe la dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 nchini India mwezi Ujao

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa

Waziri Mchengerwa amewataka wachezaji hao kuweka bidii na kufata maelekezo ya walimu huku akiwa na imani kubwa na kikosi hicho kufanya vizuri kwenye mashindano hayo pamoja na kurejea na kombe hapa nchini

''Tunawaamini sana  hakika mtakwenda kupambana na kuhakikisha mnafanya vyema katika kuitangaza nchi yetu katika mashindano hayo ni makubwa '' amesema Waziri Mchengerwa

Katika hatua nyingine Waziri Mchengerwa amemtambulisha rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Ally Mayai Tembele huku akitoa wito kwa wadau wa michezo kumpa ushirikiano ili kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini

Fainali za kombe la dunia kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 zinataraji kuanza Oktoba 11 mpaka oktoba 30,2022 huku Serengeti Girls ikipangwa kundi D pamoja na timu za Japan,Canada na Ufaransa