
Nape ametoa kauli hiyo bungeni leo, wakati ajibu swali ya nyongeza la Mbunge wa Mafinga Mjini, Mh. Cosato Chumi, ambapo amesema serikali imejipanga kutoa sapoti ya kutosha kwa timu hiyo kupitia Shirikisho la Soka nchini (TFF).
Amesema kwa mwenendendo waliouonesha vijana hao, ni dhahiri kuwa hawatakwenda Gabon kushiriki bali kuchukua ubingwa na kuwataka watanzania wote na wadau mbalimbali kushiriki kwa hali na mali katika kuiunga mkono ili kuipa nguvu.