Sebastian Vettel bado yupo yupo Aston Martin

Jumanne , 14th Sep , 2021

Sebastian Vettel anatazamiwa kusalia na kampuni Aston Martin kuelekea kwenye msimu mpya wa mashindano ya Langalanga huku Kampuni hiyo ikionesha nia yao thabiti ya kuendelea na Mjerumani huyo mpaka 2022.

Dereva wa Formula 1 kutoka Aston Martin, Sebastian Vettle.

Bingwa huyo wa dunia mara nne alijiunga na Aston Martin mwanzoni mwa msimu wa 2021 baada ya miaka sita akiwa na Ferrari. Ikiwa Vettel atachagua kuondoka atakuwa na chaguzi zingine chache ambazo ni nzuri kwani timu kubwa tayari zimeshatangaza safu kuelekea msimu ujao kitu ambacho kinaaminika kumfanya Vettel kubaki.

Muendeshaji huyo wa mbio za Formula 1, alimaliza nafasi ya pili kwenye mbio Azerbaijan Grand Prix pamoja na Hungarian Grand Prix, ingawa baadaye alivuliwa ushindi huo baada ya kugundulika hakustahili kutokana na ukiukwaji wa kiufundi wa kanuni za mashindano.

Mbio inayofuata kwenye kalenda ya F1 ni GP ya Urusi, ambayo itafanyika Septemba 26 mwaka huu.