Malengo ya timu ya Wanajangwani ni kufika nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika na safari yao itaanza kesho dhidi ya Al-Hilal S.C ambayo si timu nyepesi kutokana na historia ya timu hiyo katika mashindano ya vilabu ya CAF.Yanga SC itaingia kwenye mchezo huu ikikumbuka msimu wa 2021-2022 ambapo iliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa dhidi ya mpinzani wake wa kesho.
Kocha mkuu mpya wa klabu ya Yanga Sead Ramovic anatarajiwa kuanza kibarua chake rasmi kesho atakapoiongoza tmu yake dhidi ya Al-Hilal S.C. kutokea nchini Sudani mchezo wa makundi mzunguko wa kwanza utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa.
Ramovic kabla ya kujiunga na timu ya Wananchi alikuwa akifundisha TS Galaxy ya Afrika ya kusini,ujio wake kwa Wanajangwani umebeba matumaini makubwa kwa Wapenzi, Mashabiki na Wanachama wa Yanga baada ya timu yao kupoteza ubora wake wa msimu uliopita.
Vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Azam FC na Tabora FC vilitosha kabisa kuisukuma safu ya Uongozi wa timu hiyo bingwa mtetezi wa ligi kuu Tanzania bara na kombe la shirikisho la Tanzania kufanya maamuzi ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Angel Miguel Gamondi ili kuleta mabadiliko kwenye eneo lake la benchi la ufundi.
Malengo ya timu ya Wanajangwani ni kufika nusu fainali ya klabu bingwa barani Afrika na safari yao itaanza kesho dhidi ya Al-Hilal S.C ambayo si timu nyepesi kutokana na historia ya timu hiyo katika mashindano ya vilabu ya CAF.Yanga SC itaingia kwenye mchezo huu ikikumbuka msimu wa 2021-2022 ambapo iliondoshwa kwenye mashindano ya klabu bingwa dhidi ya mpinzani wake wa kesho.
Ramovic raia wa Ujerumani mwenye asili ya Serbia atakuwa na mtihani mgumu siku ya kesho kutokana na ukubwa wa mchezo, umuhimu wa mchezo ili kurudisha ari ya upambanaji na hali ya kujiamini iliyopotea baada ya kupoteza michezo mwili mfululizo ya ligi.Ugumu mwengine kwa upande wa Yanga kuelekea mchezo huo ni uwepo wa Kocha mwenye uzoefu mkubwa wa mashindano ya vilabu Afrika Florent Ibengé tangu akiwa na AS Vita ya Kimokrasia ya Kongo na klabu anayofundisha sasa ya Al-Hilal S.C.
Yanga SC itapaswa kuanza vizuri mchezo wake wa kwanza wa makundi kutokana na kucheza uwanja wa nyumbani ili timu ijiweke kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kucheza nusu fainali ya michezo ya CAF kwa upande wa vilabu inapaswa kushinda michezo yake yote ya nyumbani.
Sead Ramovic anamtihani wa kuhakikisha timu yake inashinda huku ikifurahisha Mashabiki wake kama walivyokuwa wakifanya watangulizi wake Nasreddine Nabi na Miguel Ángel Gamondi,Nyota huyo wa zamani wa Borussia M'gladbach ameongoza mazoezi ya kikosi chake kwa wiki mbili huku akiwakosa baadhi ya Wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza waliokwenda kuzitumikia timu zao za taifa kwenye michezo ya kufuzu AFCON 2025.
Mchezo wa kesho utatoa picha ya namna timu ya Yanga inacheza chini ya Kocha mpya, Ramovic anapswa kushinda bila kwa namna yoyote kutokana na presha iliyopo ndani ya klabu hiyo kwa sasa kama ataanza kwa matokeo ambayo Mashabiki hawatoridhika nayo inaweza kusababisha maneno ya chinichini kutoka kwa Wadau wa timu hiyo kuna watakao hoji juu ya kufukuzwa kwa Gamondi kuna watakaoulizia vigezo vilivyotumika kumpata Ramovic. Sead Ramovic hana namna nyingine zaidi ya kushinda mchezo wa kesho dhidi ya Al-Hilal S.C.