.jpg?itok=5mGWjUP0×tamp=1473334023)
Mtanzania Mbwana Samatta wa TP Mazembe ameshinda tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka anayecheza ndani ya Afrika.
Amepata tuzo hiyo katika hafla inayoendelea usiku huu jijini Lagos Nigeria ya utoaji tuzo kwa wanamichezo wa Afrika kutoka shirikisho la soka Afrika CAF.
Samatta amewashinda Robert Kidiaba wa TP Mazembe na Baghdad Bounedjah wa Etoille Du Sahel ya Tunisia.Tuzo ya jumla ya mwanasoka bora wa Afrika imekwenda kwa Pierre Emerick Aubameyang aliyepata kura 143 dhidi ya kura 136 alizopata Yaya Toure na Andrew Ayew aliyepata kura 112.
Kikosi bora cha mwaka ni:
Golikipa ni : Robert Muteba KIDIABA (DR Congo)
Mabeki ni: Serge AURIER (Cote d’Ivoire), Aymen ABDENNOUR (Tunisia), Mohamed MEFTAH (Algeria)
Viungo ni: Andre AYEW (Ghana), Yaya TOURE (Cote d’Ivoire), Sadio MANE (Senegal), Yacine BRAHIMI (Algeria)
Washambuliaji ni: Mbwana Aly SAMATTA (Tanzania), Pierre-Emerrick AUBAMEYANG (Gabon), Baghdad BOUNEDJAH (Algeria)
Tuzo ya timu bora ya taifa imekwenda kwa Ivory Coast na tuzo ya klabu bora ya mwaka imekwenda kwa TP Mazembe.
Tuzo ya kocha bora wa mwaka imekwenda kwa Herve Renard aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Ivory Coast.
Tuzo ya mwanasoka bora wa kike imekwenda kwa Gaelle Enganamouit (Cameroon)