Jumatano , 1st Jun , 2016

Nahodha na Mshambuliaji wa kimataifa wa Timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta anatarajia kuwasili saa tano usiku wa leo kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ikiwa ni maandalizi ya kuvaana na Misri jumamosi ya Juni 4.

Nahodha wa Stars, Mbwana Ally Samatta

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, Samatta alitarajiwa kuwasili mapema hii leo lakini alichelewa ndege Muscat nchini Oman hivyo ataingia usiku na kesho kujiunga na kikosi kwa ajili ya muendelezo wa mazoezi kuelekea mchezo wa jumamosi.

Lucas amesema, Mshambuliaji Thimas Ulimwengu alijiunga na kikosi jana ambapo na ameendelea na mazoezi na kikosi.

Lucas amesema, kwa upande wa Mshambuliaji wa Stars John Raphael Bocco anaendelea vizuri baada ya kuwa chini ya uangalizi wa saa 72 baada ya kuwa majeruhi huku akiendelea na mazoezi madogo madogo.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri kinatarajiwa kuwasili hii leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya wenyeji Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wa kuwania fainali za AFCON utakaopigwa jumamosi ya Juni 04 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.