
Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta (kati) aliyeruka juu akiwa na Simon Msuva(kulia) na Ibrahim Ajibu (kushoto) wakishangilia ushindi.
Samatta ndiye aliyefunga mabao yote mawili ya ushindi ya Fernebahce dhidi ya Fatih Karagumluk katika mechi ya ligi kuu nchini Uturuki iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Ikumbukwe timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars inaingia kambini leo Oktoba 5 huku baadhi ya wachezaji walioitwa na kocha Etienne Ndayiragije wamewasili kambini kujiwinda na mchezo huo.
Wachezaji wengine wa kimataifa ni pamoja na Thomas Ulimwengu anayetarajiwa kuwasili leo akitokea Congo DR, Himid Mao, Simon Msuva na Nickson Kibabage kutokea Misri na Morocco watawasili Jumatano naye Ally Msengi tayari amewasili akitokea Afrika Kusini.