Jumamosi , 3rd Nov , 2018

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Ally Samatta amepewa heshima ya kuvaa jezi maalum kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu ya Ubelgiji kati ya timu yake ya KRC Genk dhidi ya Club Brugge kutokana na kuwa kinawa wa mabao.

Zawadi ya jezi maalum aliyopewa Mbwana Samatta

Samatta atavaa jezi yenye nembo ya 'Golden Bull', jezi ambayo hukabidhiwa mchezaji anayeongoza kwa mabao katika ligi kuu hiyo ndani ya klabu ya Genk ambaye kwasasa ni Mbwana Samatta mwenye mabao 10.

Mtunza vifaa wa klabu ya Genk akiwa ameshika jezi maalum ya Samatta

Jezi hiyo amempokonya aliyekuwa kinara wa mabao kwenye timu hiyo mshambuliaji Leandro Trossard ambaye ana mabao 8 akizidiwa mawili na Samatta.

Tayari Samatta ameshakabidhiwa jezi yake hiyo na mtunza vifaa wa klabu ya Genk hivyo leo kwenye mchezo huo unaoanza saa 2:30 usiku atavaa jezi yake hiyo mpya.

ORODHA YA WAFUNGAJI
Samatta, Genk  10
Dimata,  Anderlecht  9
Santini, Anderlecht 9
Trossard, Genk8
Harbaoui, Waregem 7
Malinovsky, Genk 7
Wesley,  Club Brugge 7