
Winga wa Arsenal B
Saka ambaye ni winga wa kushoto wa timu ya soka ya Arsenal amekuwa na msimu mzuri hadi kumshawishi kocha mkuu wa timu ya Taifa ya England Gareth Southgate kumteua katika kikosi cha hivi karibuni, kinachojiandaa na michezo mitatu tarehe 8/10/2020 Wales, 11/10/2020 Belgium na 14
/10/2020 Denmark.
''Sio jambo geni kwetu , tumekuwa na wachezaji wengi wenye asili ya mataifa mengine, lakini wamezaliwa hapa England, Saka ni mchezaji mwenye umri mdogo ana vitu vya kujifunza hapa, na pia ana muda mrefu wa kucheza katika timu ya Taifa kama akizingatia'' alisema Southgate
Saka kwa sasa ana umri wa miaka 19 tu hivyo, anatazamiwa kucheza kwa muda mrefu, japo mjadala mkubwa ni kama ataendelea kupata nafasi kwenye timu ya Taifa ya England kutokana na taifa hilo kuwa na wachezaji wengi nyota na kizazi kingine kikubwa kinachochipukia kwenye vikosi vya timu ya taifa za vijana.
KWANINI SAKA NI MUHIMU KWA MATAIFA HAYA MAWILI?
Kiwango alichokionesha msimu huu kimewavutia wengi michezo 45 aliyocheza ikiwa na jumla ya dakika 3084 ametoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Arsenal hasa kwenye mafanikio vya kutwaa ubingwa wa FA na Ngao ya Jamii. Nigeria walimuhitaji kama mrithi wa wachezaji wao wakongwe ambao umri unawatupa mkono akiwemo Ahmed Musa.