Sabalenka mwenye umri wa miaka 26 ni mshindi wa mataji mawili makubwa ya tenisi mwaka kwa mwaka 2024 yani Grand Slams. Ameshinda ubingwa wa michuano ya wazi ya Australia Australian Open na Michuano ya wazi ya Marekani US Open.
Aryna Sabalenka ameweka wazi kuwa sababu ya kushiriki michuano hii ya wazi ya china ni kwasababu anataka kukusanya alama nyingi zadi zitakazomfanya awe namba 1 kwa ubora Duniani hasa ukizingatia mchezaji namba moja kwa ubora Duniani Iga Swiatek ambaye pia ni bingwa wa michuano hii hatashiriki kwenye michezo ya China Open.