Kabla ya mchezo wa jana tayari timu hizo zilikuwa zimeshakutana mara nne kwenye michuano ya FA na kati ya hizo Wigan walishinda mara mbili ikiwemo fainali ya kombe hilo mwaka 2013 kwa bao lilofungwa na Ben Watson.
Pamoja na hayo lakini pia Wigan walikuwa na rekodi nzuri ya kushinda michezo yao sita ya mwisho ya Kombe la FA kwenye uwanja wao wa nyumbani hivyo haikuwa ajabu kubwa kuwafunga Manchester City.
Kwa upande wa Manchester City walikuwa wanajivunia rekodi yao ya kutoruhusu goli kwenye michuano hiyo tangu wapoteze 5-1 dhidi ya Chelsea kwenye dimba la Stamford Bridge katika mechi ya raundi ya tano ya FA mwaka 2016.
Mchezo wa jana ulimalizika kwa Wigan kushinda bao 1-0 hivyo kuwatupa nje ya michuano hiyo vinara wa ligi kuu soka ya England Man City huku wakiwa timu ya pili kuifunga timu hiyo msimu huu wakitanguliwa na Liverpool waliowafunga 4-3 kwenye mchezo wa EPL.
