Donald Ngoma akiwa kwenye moja ya mechi za Azam FC
Mtendaji Mkuu wa Azam FC Abdulkarim Amin ameongea na Kipenga ya East Africa Radio inayoruka kila siku Saa 2:00 - 3:00 usiku na kuthibitisha kuwa wameachana na Ngoma kufuatia mkataba wake kumalizika Juni 15, 2020.
Ngoma alijiunga na Azam akitokea Yanga miaka miwili iliyopita lakini akapata majeraha ambayo yalimlazimu kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu sana.
Kwa mwendelezo zaidi usikose Kipenga ya East Africa Radio kuanzia Saa 2:00 - 3:00 usiku.



