Rudy Gobert mlinzi bora, Harden pancha NBA

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Nyota wa timu ya Utah Jazz, Rudy Gobert amefanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya mlinzi bora wa ligi ya kikapu nchini Marekani kwa msimu huu 'NBA KIA Defensive player of the year' baada ya kuwapiku Draymond Green wa Golden State Warriors na Ben Simmons wa Philadelphia 76ers.

Mlinzi wa Utha Jazz, Rudy Gobert akitupi ampira kwenye kikapu.

Rudy alipata kura 464 na kuibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mara ya tatu baada ya kutwaa msimu wa mwaka 2017-2018 na 2018-2019 wakati Draymond Green akiambulia kura 287 na Ben Simmons akiondoka na kura 76 pekee.

Kwa upande mwingine:

Nyota wa Brooklyn Nets, James Harden ataendelea kukosekana kwenye mchezo wa saa nane usiku wa kuamkia kesho dhidi ya Milwaukee Bucks baada ya nyota huyo kuendelea kusumbuliwa na maumivu ya misuli hivyo nafasi yake kuchukuliwa na mlinzi Joseph Harris.

Mchezo mwengine wa mzunguko watatu wa hatua ya Nusu fainali ya NBA kwa ukanda wa Mashariki utakaochezwa usiku wa kuamkia kesho ni ule utakaowakutanisha Utah Jazz watakaokipiga na Los Angeles Clippers saa11:00 Alfajiri.