Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Boniface Wambura amesema, michuano hiyo inamalizia hatua ya mzunguko ambapo mpaka sasa zimepatikana timu mbili ambapo baada ya kumaliza hatua ya mzunguko, zitapatikana timu mbili ambazo zitaungana na sita zilizopatikana na kufanya timu kuwa jumla ya nane.
Wambura amesema, timu zote zinatakiwa kuwasili jijini Dar es salaam Januari 25 kwa ajili ya kuanza michuano hiyo ambapo michuano itaanza siku inayofuata na hatua ya Fainali itafanyika Februari Mosi jijini
Dar es salaam.
Wambura amesema hadi sasa timu zilimaliza hatua ya mzunguko na kufanikiwa kuingia hatua ya Robo fainali ni Ilala, Pwani,Temeke, Mwanza, Tanga na Kigoma huku timu ambazo bado hazijamaliza hatua ya mzunguko ambazo zinamalizia leo ni Iringa ikikutana na Ruvuma huku Mbeya ikicheza na katavi.