
Wanariadha...
Katibu msaidizi wa Chama cha Riadha visiwani Zanzibar Mlingi Bwire amesema, suala la kuweka ushirikiano kati ya wao na (RT) siyo suala la kutumia nguvu kwani ni suala la kuelewana na itasaidia kwa kiasi kikubwa Wazanzibar kuweka imani katika mchezo huo pamoja na vijana kuwa na uwezo wa kushiriki hata mashindano ya kimataifa.
Bwire amesema, Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Baraza la Michezo Zanzibar (BMZ) wangekutana pia kwa ajili ya kuweka sawa suala hilo.
Chama cha Riadha Tanzania (RT) kilifanya uchaguzi wake mkuu hapo jana na kuwapata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho kwa miaka minne ijayo.
Katika uchaguzi huo Anthony Mtaka alichaguliwa kuwa Rais, William Kalaghe (Makamu wa Rais - Utawala), Dk Ahmed Ndee (Makamu wa Rais - Ufundi), Wilhelm Gidabuday (Katibu Mkuu), Ombeni Zavala (Katibu Mkuu Msaidizi) na Gabriel Liginyani (Mweka Hazina).
Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lwiza Msyani, Meta Bare, Rehema Killo, Dk Nassor Matuzya, Robert Kalyahe, Zakaria Buru, Mwinga Sote, Tullo Chambo, Christian Matumbo na Yohana Mesese.