Jumatatu , 5th Oct , 2020

Raundi ya tano ligi kuu soka Tanzania bara inakamilishwa leo kwa mchezo mmoja katika dimba la Uhuru Jijini Dar es salaam, ambapo klabu ya KMC watakuwa wenyeji wa Polisi Tanzania.

Msimu uliopita KMC walipoteza michezo yote miwili ya ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania

KMC wanarejea jijini Dar es salaam baada ya kucheza michezo miwili ugenini kanda ya ziwa, ambako walishinda mchezo mmoja dhidi ya Mwadui FC kwa bao 2-1 na mchezo mwingine walipoteza dhidi ya Kagera Sugar kwa bao 1-0.

Wanakutana na Polisi Tanzania ambao hawajapoteza mchezo katika michezo mitatu iliyopita, wameshinda michezo miwili na wametoka sare mchezo mmoja, na mchezo wa mwisho wameshinda 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC.

Msimu uliopita Polisi Tanzania walishinda michezo yote miwili dhidi ya KMC, mchezo wa kwanza katika uwanja wao wa nyumbani wa Ushirika Moshi walishinda 2-1, na mchezo wa pili katika dimba la Uhuru Dar es salaam walishinda 3-2.

Tofauti yao kwenye msimamo wa ligi ni alama 2 tu KMC wapo nafasi ya 6 wakiwa na alama 9 wakati Polisi Tanzania wapo nafasi ya 7 wakiwa na alama 7.

Mchezo huu wa mwisho wa raundi ya tano unachezwa majira ya Saa 10:00 Jioni.

Matokeo ya michezo ya raundi ya tano iliyochezwa.

IJUMAA

Dodoma Jiji FC 2 – 0 Ruvu Shooting

JUMAMOSI

Gwambina FC 2 - 0 Ihefu FC

Namungo FC 0 - 1 Mwadui FC

Mbeya City FC 0 - 0 Tanznaia Prisons

Yanga SC 3 – 0 Coastal Union

JUMAPILI

Biashara United 1 - 0 Mtibwa Sugar

JKT Tanzania 0 – 4 Simba SC

Azam FC 4 - 2 Kagera Sugar