Ijumaa , 4th Jan , 2019

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera amefanya mabadiliko ya uongozi kwenye kikosi chake kwa kumvua kitambaa cha unahodha mlinzi Kelvin Yondani na kumkabidhi mshambuliaji Ibrahim Ajibu.

Ibrahim Ajibu

Zahera amefikia uamzi huo baada ya Kelvin Yondani kuwa mtovu wa nidhamu kwa kuchelewa kuripoti kambini baada ya siku 5 za mapumziko kuisha bila yeye kuonekana wala kutoa taarifa. 

''Nilitoa siku 4 za mapumziko baada ya mechi na Mbeya City lakini yeye kama nahodha hakuripoti kambini baada ya siku hizo na hajatoa taarifa yoyote ndio maana nimeamua Ajibu awe nahodha mpya wa timu'', amesema.

Kikosi cha Yanga SC kilichobakia Dar es Salaam leo hii kimenza mazoezi kwenye viwanja vya Polisi Kurasini baada ya mapumziko ya siku nne. Wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza pamoja na wale wa U20 wapo Zanzibar kushiriki michuano ya Mapinduzi Cup.

Yondani na Ajibu wote waliwahi kuichezea klabu ya Simba ambapo Yondani alijiunga na Yanga akitokea Simba mwaka 2013 huku Ajibu akijiunga na Yanga mwaka 2017.