Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt.Damas Ndumbaro akiwakabidhi fedha hizo wachezaji hao kwenye makao makuu ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF ) ikiwa ni zawadi wa timu hiyo.
Ndumbaro amewataka wachezaji hao kujituma na kupambana na kuweza kupata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa kwa ajili ya kujenga timu ya taifa imara ya wanawake.
“Rais Samia amefurahishwa sana na ushindi huo na kutoa zawadi ya mama kwa kutoa kiasi cha Mill 30, kwa kuwakabidhi 10 na kesho (Alhamisi, Agosti 12) tutawamalizia 20 kwa sababu mfumo umetukwamisha,” amesema.
Kwa upande wa Nahodha wa timu hiyo Jamila Rajabu ametoa shukran kwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa motisha hiyo huku wauahidi kufanya vyema katika mashindano ya wanawake ya kufuzu kushiriki kombe la dunia