Pre season ya Simba imesheheni

Jumatano , 15th Sep , 2021

Kwa ripoti za awali wachezaji wa Simba walianza kuripoti kambini Agosti 8, kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, tayari kwa vipimo kwa wachezaji wapya na wale wa zamani pamoja na kupewa vifaa vya kutumia kwenye Pre-season, baada ya hapo kikosi kiliondoka kwenda Moroco Agosti 10, 2021,

Kikosi cha Simba SC

Agosti 12, 2021 Simba ilifanya Mazoezi ya kwanza wakiwa Morocco, lakini pia wakiwa huko walicheza michezo miwili ya kirafiki, dhidi ya AS Far Rabat 2-2 Simba SC na Olympique Club 1-1 Simba SC zote za Morocco na Agosti 29 kikosi hicho kilirejea nchini.

Lakini pia Mabingwa hao wa Tanzania bara waliporejea nchini hiyo Agosti 29 walielekea Arusha ambako wameweka kambi huko ikiwa ni muendelezo wa Pre-Season yao, kabla ya kurejea Dar es salaam tayari kwa tamasha la Simba Day Septemba 19, 2021, huko nako wamecheza michezo mitatu ya kirafiki, dhidi ya Coastal Union 0-0 Simba SC, Simba SC 1-0 Fountain Gate na Simba SC 2-1 Aingle Noir, lakini pia idadi hiyo ya michezo itaongezeka kwani wanamchezo dhidi ya TP Mazembe Septemmba 19 kwenye tamasha la Simba Day kwenyedimba la Benjamini mkapa.

Na mchezo wa kwanza wa mashindano kwa Simba msimu huu utakuwa dhidi ya watani zao Yanga SC kwenye mchezo wa ngao ya Jamii utakao chezwa Septemba 25 katika dimba la Benjamini mkapa Dar es salaam.

Toka Agosti 8, 2021, Simba ilipoanza maandalizi ya msimu mpya katika zoezi la upimaji afya mpaka leo Septemba 15 2021, zimetimia siku 39 tangu kikosi hicho kianze kujiandaa.

Simba wamecheza jumla ya michezo mitano (5) ya kirafiki,

AS Far Rabat 2-2 Simba SC
Olympique Club 1-1 Simba SC
Coastal Union 0-0 Simba SC
Simba SC 1-0 Fountain Gate
Simba SC 2-1 Aingle Noir