
Nonga amesaini mkataba wa miaka miwili akitokea Mwadui FC, ambayo ameichezea kwa miezi mitano tu tangu ajiunge nayo kutoka Mbeya City.
Naye mchezaji huru kutoka Niger, Issoufou Boubacar Garba amesaini Mkataba wa mwaka mmoja, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja, iwapo atafanya vizuri.
Garba alitua klabu ya African mwaka 2012 ya Tunisia ambako hakucheza mechi hadi anahamishiwa ES Hammam-Sousse ambako pia hakucheza huku wasifu wake unaonesha tangu ameondoka ES Hammam-Sousse hajapata timu nyingine, lakini uongozi wa Yanga SC umejiridhisha alikuwa anachezea klabu bingwa ya kwao, AS Douanes.