Alhamisi , 20th Mar , 2014

Jeshi la polisi nchi limesema kuwa linafanya uchunguzi juu ya kifo cha shabiki wa soka ambaye alifariki baada ya kuanguka ghafla uwanjani, wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, baina ya mabingwa watetezi Yanga na vinara wa ligi Azam

Kamishna wa polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam, Kamanda Suleiman Kova amesema kuwa awali wakati mechi ikiendelea, shabiki huyo Deodatus Isaya mwenye miaka 48 mkazi wa kipunguni A jijini Dar es salaam alianguka ghafla na kuonekana kama amezirai, lakini baadae aligundulika amekwishafariki

Kamanda Kova ameongeza kusema kuwa, baada ya uchunguzi huo kwa kushirikiana na madaktari watatoa majibu ya kile kilichomsibu shabiki huyo na kusababisha kifo chake.