Kocha mpya wa Manchester City Pep Guardiola.
Baada ya kuvutiwa na uwezo wa mshambuliaji nyota wa Celta Vigo Nolito kocha mkuu wa matajili wa jiji la Manchester timu ya Manchester City Pep Guardiola sasa amedhamiria kumtwaa kiungo huyo ambaye anaiwakilisha nchi yake katika michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa kwa sasa.
Manchester City wanataka kuizidi kete timu ya Barcelona na kumsajili mshabuliaji huyo ambaye anamagoli matano na kutengeneza manne katika michezo 12 ya kiataifa aliyoichezea Hispania mpaka sasa.
Nilito mwenye miaka 29 ataondoka Celta Vigo msimu huu na Pep Guardiola pamoja na mataikuni Txiki Begiristain wanajiandaa kufanya kilalinalowezekana kuhakikisha mshambuliaji huyo anatua Etihad ambapo inakadiriwa kuwa samani ya uhamisho wake ni kiasi cha pauni milioni 14.1.
Hispania imekuwa ikicheza na kina David Silva, Alvaro Morata na Nolito katika eneo la ushambuliaji na Guardiola anataka Silva, Sergio Aguero, Nolito wawe pacha watatu wakuongoza safu ya ushambuliaji ya Man City.
Kwa sasa inabidi wajipange sawasawa hasa baada ya mchezaji huyo kuivutia pia Barcelona ambayo ni moja ya timu kubwa ambayo kila mchezaji angependa kucheza katika timu hiyo hivyo ni wazi Man City wanakabiliwa na upinzania wakutosha kumnasa mchezaji huyo ambaye aliwahi kutakiwa na Barcelona mwezi Januari mwaka huu lakini dili halikukamilika baada ya Barca kushinda ada ya uhamisho wake wakati huo.
Wakati huo huo Manchester City katika hali ya kutaka kuongeza ushindani katika nafasi ya golini amabyo hivi sasa inashikiliwa na kipa wa England Joe Hart timu hiyo inataraji kumpa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja kipa wa zamani wa Fc Barcelona aliyejiunga Manchester United Victor Valdes mwenye miaka 34 ambapo kwa sasa yuko huru baada yakumaliza mkataba wake na United.