
Nahodha msaidizi wa Polisi Tanzania akizungumza na EATV akiwa mazoezini.
Akizungumza na Eatv Nahodha huyo wa Maafande wa Polisi Tanzania amesema kwa sasa anacheza vizuri sababu ya kuaminiwa na hana shinikizo kama amabavyo ilikuwa awali na hii imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa baadhi ya wachezaji ambao wanapita hususani vilabu vya Simba, Yanga, Azam.
''Uzoefu niliopata wakati nikiwa kwenye klabu ya Yanga umenifanya kuwa beki mzuri na ninayeaminiwa na bechi la ufundi la polisi Tanzania na kuniona nafaa kuwa nahodha msaidizi wa timu hiyo'' amesema nahodha Polisi Tanzania Pato Ngonyani.
Katika hatua nyingine Pato Ngonyani amesema yuko tayari kurudi kwenye timu yoyote ikiwepo timu yake ya zamani kama kutakuwa na maslahi kwa kuwa mpira ni maisha yake.