Jumanne , 16th Feb , 2016

Bondia na Mwanasiasa wa Ufilipino Manny Pacquiao ameomba radhi kwa kile kilichozuia taharuki kwa watu mara baada ya kutamka kuwa wapenzi wa jinsia ni "wabaya zaidi ya wanyama".

Bondia na Mwanasiasa wa Ufilipino Manny Pacquiao ameomba radhi kwa kile kilichozua taharuki kwa watu mara baada ya kutamka kuwa wapenzi wa jinsia moja ni "wabaya zaidi ya wanyama".

Akiandika kwenye ukurasa wake wa facebook, Pacquiao alisema bado atapinga ndoa za mashoga lakini hakulaani.
"Mungu awabariki nyote na ninawaombea,"Aliongeza

Katika mahojiano ya moja kwa moja kwenye runinga ya taifa, bondia huyo alizua mjadala mkali na majibizano kati ya wanaharakati wa kupigania haki za wapenzi wa jinsia moja na umma.

Bondia huyo bingwa wa zamani wa uzani wastani duniani ni mkristo imara ambaye anawania kiti cha useneta katika uchaguzi mkuu ujao unaoratibiwa kufanyika mwezi Mei.

Ufilipino inatajwa kuwa asilimia kubwa ya wakatoliki ambao wanapinga kimya kimya mapenzi ya jinsia moja.

Mbunge huyo ( Pacquiao), alikuwa akihojiwa katika runinga ya TV5 mapema hapo jana.

Video inayoonesha wakati alipotamka maneno hayo katika lugha ya Tagalog, inamuonesha bondia huyo akisema

"Ni ukweli usiopingika kuwa wanyama ambao tunawafuga wanaheshimu maadili kuna ya kiume na ile ya kike'' .

''Je ushawahi kuona mnyama wa kiume akimkurubia mwenzake wa kiume ?''

''Au hata mnyama wa kike akimpandilia yule wa kike ?''

''Haiwezekani ?

''Kwa hivyo wanadamu wamegeuka na kuwa wabaya hata kuwazidi wanyama''!