Juuko Murshid, Beki wa Simba SC
Juuko yupo kwao Uganda na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, The Cranes ambacho kitashiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani nchini Gabon.
Omog raia wa Cameroon anaamini chini ya ukuta wa mabeki wa kati, Banda na Method Mwanjale timu yake haitafungwa mabao ya ajabu kama ilivyokuwa katika mzunguko wa kwanza.
Omog alisema safu yake ya ulinzi aliyoifanyia mabadiliko hivi karibuni kwa kumpatia nafasi ya kucheza mchezaji wake kiraka, Abdi Banda kama beki wa kati akishirikiana na Mwanjale inafanya vizuri.

Abdi Banda akipongezwa baada ya kuifungia Simba bao katika moja ya michezo yake
Alisema Banda anafanya majukumu makubwa ambayo hapo awali walinzi wa kati wa timu hiyo walikuwa hawayafanyi kama vile kucheza mpira yote ya vichwa na ile ya chini kwa ustadi mkubwa.
“Baada ya kutokuwa na Juuko kulikuwa na tatizo la umakini lakini sasa baada ya kumpatia nafasi Banda naona umakini umeongezeka na anafanya vizuri zaidi kwa kucheza mipira ya vichwa ambayo ilikuwa ni tatizo kubwa kwetu.
“Kutokana na hali hiyo, sasa sitegemei kuona tunafungwa mabao ya ajabu lakini pia hivi sasa najitahidi sana kuhakikisha safu yetu ya ushambuliaji nayo inakuwa moto wa kuotea mbali,” alisema Omog.





