Manuel Nolito(pichani)akishangilia bao akiwa na timu yake ya Taifa ya Hispania.
Nolito mwenye umri wa miaka ishirini na tisa amesaini mkataba wa miaka minne kuitumikia Manchester City na sasa anaungana na kocha wake Pep Guardiola aliyefanya naye kazi pamoja katika klabu ya Barcelona tangu mwaka 2008 hadi 2011.
Nyota huyo alijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa kilichokuWa kikishiriki michuano ya mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa baada ya kazi nzuri aliyoifanya msimu uliopita akiwa na klabu yake kwa kuifungia mabao kumi na mbili msimu uliopita wa La Liga.
Manchester City imemkabidhi nyota huyo jezi namba tisa na sasa anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na kocha Pep Guardiola akiwemo kiungo Ilkay Gundogan kutoka Borussia Dortmund.

