Jumatano , 3rd Dec , 2014

Mashindano ya ngumi ya Taifa yameanza leo jijini Dar es Salaam yakishirikisha vilabu 15 hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio Mwenyekiti wa Mashindano kotoka shirikisho la ngumi za ridhaa nchini BFT Anthony Mwang'onda amesema mashindano hayo yenye lengo la kutafuta timu ya Taifa yatafanyika kwa muda wa siku Saba.

Mwang'onda amesema katika mashindano hayo wataunganisha na kumbukumbu ya kumuenzi Rais wa zamani wa Afrika Kusini Hayati Nelson Mandela aliyefariki desemba 5 mwaka uliopita, ambaye pia alikuwa bondia wakati wa ujana wake.