Alhamisi , 17th Apr , 2014

Kocha wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes John Simkoko amesema kikosi chake kiko imara tayari kupambana na Kenya katika mechi ya marudiano ya mchujo kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.

Wachezaji wa Ngorongoro mara baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya Kenya na kutoka 0-0 jijini Nairobi,Kenya

Kocha wa timu ya taifa ya vijana walio na umri chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes John Simkoko amesema kikosi chake kiko imara tayari kupambana na Kenya katika mechi ya marudiano ya mchujo kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana itakayofanyika mwakani Dakar nchini Senegal.

Mechi hiyo ya marudiano itapigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam tarehe 27 April mwaka huu,timu hizo zilitoka sare tasa zilipokutana majuma mawili yaliyopita jijini Nairobi nchini Kenya.

Timu hiyo inaendelea na kambi tayari kwa ajili ya mpambano huo wa marudiano, mtanange utakayopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.