
Niyonzima amesema kuwa nje ya klabu yake ya Yanga anavutiwa sana na uchezaji wa kiungo wa Simba Said Hamisi Ndemla na kusema ndani ya klabu yake ya Yanga anamkubali sana Kelvin Yondani ambaye ni rafiki yake mkubwa, pia Niyonzima alidai kama akiwa kocha mchezaji wa kwanza kumsajili katika timu lazima atakuwa Kelvin Yondani wa Yanga.
Mbali na hilo kiungo huyo wa Yanga alisema katika muziki wa bongo fleva msanii anayemkubali na kupenda sana kazi zake ni Alikiba ambaye sasa hivi anafanya vyema na remix yake ya 'Aje'