Ijumaa , 1st Apr , 2022

Nyota wa mchezo wa Tennis raia wa Japan Naomi Osaka amefanikiwa kumshinda Belinda Bencic katika mchezo wa Nusu fainali ya michuano ya Miami Open, na kutinga hatua ya fainali ambapo atacheza dhidi ya mchezaji anayetajwa kupanda kwa kasi katika mchezo huo Iga Swiatek wa Poland.

(Naomi Osaka)

Osaka alimtupa nje Belinda Bencic wa Uswizi kwa ushinda wa Seti tatu kwa alama 4-6, 6-3, 6-4 na kutinga fainali yake ya kwanza tangu ashinde Australian Open mwaka 2021. Sasa Naomi ameorodheshwa katika nafasi ya 77 duniani huku akiendelea kurejea taratibu kataika nafasi za juu akitokea mapumzikoni.

Swiatek alishinda taji la michuano ya Indian Wells wiki iliyopita dhidi ya Mmarekani Jessica Pegula kwa alama 6-2 na 7-5 na kuwa mchezaji wa kwanza kufika fainali ya mashindano yote miwili ya Marekani tangu Victoria Azarenka afanye hivyo, ambaye alishinda mashindano yote mawili mwaka wa 2016.

Swiatek na Osaka hajakutana tangu mwaka 2019, ambapo Osaka alishinda kwa seti za moja kwa moja, lakini tangu wakati huo amefanikiwa kushinda taji moja tu la Grand Slam kwenye 2020 French Open.