Ijumaa , 15th Jun , 2018

Siku chache baada ya kuundwa kwa kamati ya mpito ya kuivusha Yanga katika kipindi kigumu walicho nacho, Mwenyekiti wa kamati hiyo Abasi Tarimba amefunguka kuhusu masuala ya usajili ndani ya klabu hiyo.

Tarimba aliyekabidhiwa mwenyekiti wa kamati hiyo, ameeleza zaidi namna watakavyofanya kazi na hali halisi ya usajili ndani ya klabu hiyo huku akitamba kuwa Yanga itarejea kama zamani na wanasajili kimya kimya.

"Tupo katika kipindi kigumu na kila mtu anajua ila tutapambana kuhakikisha tunarejesha hadhi ya Yanga, tutasajili kimya kimya na kwa weledi wa hali ya juu", amesema Tarimba.

Ameongeza kuwa  "Klabu zote zinajua kuwa Yanga hawakoseagi katika usajili ndiyo maana tukitaja tuu jina la mchezaji wanakimbilia kumsajili sasa mambo yatafanyika kimya kimya" .

Yanga iliunda kamati hiyo katika mkutano mkuu wa klabu hiyp uliofanyika Juni 10 mwaka huu na kuadhimia kufanya mabadiliko ya uendeshaji ndani ya klabu hiyo kongwe nchini Tanzania.