Jumatano , 9th Jun , 2021

Maurizio Sarri ametangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya SSC Lazio inayoshiriki ligi kuu Italia maarufu Serie A kwa kipindi cha miaka miwili hadi 2023.

Maurizio Sarri kocha mpya wa SSC Lazio

Sarri hakuwa na timu tangu alivyoondolewa Juventus baada ya msimu wa mwaka 2019-2020 ambapo wamiliki wa timu hawakuridhishwa na kiwango chake cha ufundishaji licha ya kuwapa ubingwa wa serie A, lakini aliondolewa kwa kigezo cha kutofanya vizuri katika kombe la mabingwa wa Ulaya alipotolewa hatua ya 16 bora dhidi ya Real Madrid.

Kocha huyu mkongwe mwenye umri wa miaka 62 raia wa Italia aliyeanza ufundishaji wa soka mwanzoni mwa miaka ya 1990 , amevifundisha vilabu 20 mbalimbali ikiwemo Napoli, Chelsea, Juventus huku klabu ya Lazio ikiwa ni ya 21 katika historia yake ya ufundishaji soka.

Sarri si kocha mshindi katika historia yake, pamoja na kuwepo kwa muda wa miaka 30 kwenye ufundishaji ambapo mpaka sasa ameshinda kombe moja tu la Serie A akiwa na Juventus katika msimu wa 2019/2020