Andy Murray(pichani) akionyesha umwamba wake uwanjani
Murray ametinga hatua hiyo baada ya hapo jana kumshinda mu-Australia Nick Kyrgios kwa seti 7-5 6-1 6-4 na kutinga robo fainali ya tisa ya michuano hiyo.
Wakati huohuo madada wawili ndugu Venus na Serena Williams kwa mara nyingine tena wameendelea kuonesha kuwa umri siyo kikwazo kwa kuwa wanasalia kama kitisho katika Wimbledon.
Serena mwenye umri wa miaka thelasini na nne ambaye pia ndiye bingwa mtetezi upande wa wanadada atakutana na mrusi Anastasia Pavlyuchenkova katika robo fainali hiyo.


