Jumapili , 9th Nov , 2014

Mechi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar iliyoahirishwa hapo jana baada ya mvua kubwa kunyesha imemalizika leo hii kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kutoa sare ya bao 1-1.

Akizungumza na East Africa Radio, Msemaji wa Timu ya Mtibwa Sugar Thobias Kifaru amesema Mtibwa Sugar ndiyo ilianza kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 43 ambapo goli hilo lilidumu hadi kipindi cha mapumziko lakini mchezo huo ulisimamishwa baada ya kutokea kwa hali ya mvua.

Kifaru amesema katika kipindi cha pili cha mchezo huo kilichochezwa leo asubuhi Kagera Sugar ilifunga moja hivyo kudumu mpaka kuisha kwa mchezo na kupelekea kwa timu hizo kutoa sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar kuendelea kuongoza Ligi kuu kwa kuwa na Pointi 15.