Jumatatu , 12th Oct , 2015

Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.Juliana Yasoda amekabidhi bendera kwa timu za taifa za Tanzania wanaume na wanawake mchezo wa mpira wa magongo (Hockey) tayari kwa safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini.

Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi.Juliana Yasoda amekabidhi bendera kwa timu za taifa za Tanzania wanaume na wanawake mchezo wa mpira wa magongo (Hockey) tayari kwa safari ya kuelekea nchini Afrika Kusini katika mashindano ya Afrika kufuzu kwenda michezo ya Olympic mwakani nchini Brazil.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo katibu mkuu wa chama cha mpira wa magongo mkoa wa Dar es Salaam Mnonda Magani amesema timu hizo zitakuwa na jumla ya wachezaji 24 na viongozi wa nne,ambapo hadi sasa maandalizi yanaendelea vizuri kuelekea kwenye mashindano.

Naye nahodha wa timu ya taifa kwa upande wa wanawake Kidawa Selemani amesema kuwa wamejiandaa kikamilifu kupambana na timu za Zimbabwe, Afrika kusini na Zambia na ana imani watafuzu kuelekea Brazil mwakani.

Timu hizo zinataraji kuondoka nchini Oktoba 19 mwaka huu kuelekea nchini Afrika Kusini ambapo mashindano hayo yataanza rasmi Oktoba 25 jijini Johanesburg.