Jose Mourinho akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Manchester, akiwa na kikosi chake wakitokea China, Alfajiri ya leo
Manchester United, imerejea alfajiri ya leo, nchini Uingereza ikitokea China, baada ya kujikuta ikicheza mechi moja tu ya kirafiki nchini humo, kuliko vile walivyopanga.
Mchezo wa Debry na mahasimu zao, Manchester City uliokuwa upigwe jana jijini Beijing umeahirishwa baada ya mvua kubwa kunyesha na uwanja wa Bird's Nest kujaa maji.
Kabla ya hapo, kikosi cha Jose Mourinho, kimejipima kwa mechi moja ya kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Borussia Dortmund mjini, Shanghai, ijumaa iliyopita.


