Jumanne , 5th Mei , 2020

Mchezaji wa Timu ya Kagera Sugar Kelvin Sabato, amesema Mshambuliaji wa Yanga David Molinga ni moja ya washambuliaji ambao wana kiwango kikubwa cha uchezaji licha ya kukosolewa na mashabiki wa mpira.

Mchezaji wa Timu ya Kagera Sugar Kelvin Sabato na David Molinga

Kelvin Sabato amesema hayo wakati wa kipindi cha #KipengaXtra cha East Africa Radio, ambapo amesema endapo Molinga akipewa nafasi atafanya vizuri kwenye kikosi cha Yanga.

"Mimi ni mshambuliaji na huwa ninategemea sana nafasi ninazo tengenezewa na watu waliokuwa nyuma yangu, kwa mimi binafsi Molinga anajua mpira na vitu vingi sana anavyo muhimu je waliokuwa nyuma yake wanamtengenezea nafasi?" amesema Kelvin Sabato.

Tazama zaidi.