Alhamisi , 26th Jan , 2017

Kiasi cha pauni laki 3 (Zaidi ya Tsh. milioni 837) kimechangishwa kwenye mchezo wa kirafiki, pale Brazil ilipoifunga Colombia 1-0 katika mchezo wa kusaidia familia za wachezaji na wafanyakazi wa klabu ya Chapecoense waliofariki kwenye ajali ya ndege.

Wachezaji wa Brazil wakimfariji aliyekuwa golikipa wa Chapecoense Follman ambaye ni mmoja wa manusura wa ajali ile

 

Katika mchezo huo uliopigwa alfajiri ya leo kwa masaa ya Afrika Mashariki, mshambuliaji, Dudu aliwafungia Brazil bao kabla ya mapumziko, katika uwanja wa Olimpiki mjini Rio.

Chapecoense walitoka 2-2 na Palmeiras, kwenye mchezo wa kirafiki Jumamosi iliyopita ikiwa na kikosi kipya kilichosajiliwa baada ya miezi miwili ya kupoteza wachezaji wake kwenye ajali iliyotokea mwezi Novemba mwaka jana.

Watu 6 pekee ndiyo waliobaki katika msafara wa watu 77 waliokuwemo kwenye ndege ya  LaMia iliyobeba wachezaji wa Chapecoense ikielekea Colombia kucheza fainali ya Copa Sudamericana.