Jumapili , 11th Nov , 2018

Jumapili ya Novemba 11, Real Betis imeka historia kuwa timu ya kwanza ya kufunga mabao manne dhidi ya Barcelona katika dimba la Camp Nou katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Lionel Messi

Barcelona imekubali kichapo cha mabao 4-3 katika uwanja wake wa nyumbani mbele ya Real Betis siku ya Jumapili ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kukubali kufungwa mabao manne katika uwanja wake wa Camp Nou katika miaka 15.

Katika mchezo huo, Lionel Messi alionekana kwa mara ya kwanza tangu alipoumia bega la mkono wake kwenye mchezo dhidi ya Sevilla mnamo Oktoba 20 , alifunga mara mbili, lakini hayakuweza kutosha kuzuia kichapo hicho kutoka kwa vijana wa Real Betis.

Barca iliruhusu mabao kutoka kwa Junior, Joaquin, Giovani Lo Celso na Sergio Canales, ambapo ni kwa mara ya kwanza imekubali kufungwa mabao hayo manne nyumbani tangu ilipofunga 4-2 dhidi ya Deportivo La Coruna mwezi Aprili 2003.

Barca imeendelea kubaki juu ya msimamo wa LaLiga, lakini majirani wao Espanyol wanaweza kuwa sawa nao kwa pointi 24 ikiwa watashinda dhidi ya Sevilla usiku wa Jumapili.