Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi akionyesha uwezo wake uwanjani.
Tuzo hiyo ilitolewa msimu wa 2013-2014, lakini Messi ambaye ni mchezaji bora wa dunia mara tano alikuwa hajashinda tuzo katika mara 22 ambazo imetolewa.
Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 28, hatimaye ametuzwa baada ya kufunga mabao matano katika mechi sita alizocheza mnamo mwezi Januari.
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ameshinda tuzo hiyo mara mbili tangu ianzishwe mnamo mwezi Septemba 2013.
Wachezaji wa Atletico Madrid Diego Godin na Antoine Griezman, pamoja na mshambuliaji wa Real Sociadad Carlos Vela pia wameshinda mara mbili.
Messi ni mchezaji wa pili katika klabu ya Barcelona kushinda taji hilo baada ya Neymar mnamo mwezi Novemba mwaka jana.





