
Mecky Mexime, mkuu wa kituo cha kukuzia vipaji vya soka 'Cambiasso Sports Management'.
Akizungumza Jijini Dar es salaam , wakati wa utambulisho huo Kocha Mexime amesema watachagua wachezaji wenye vipaji ambapo pia watazunguka mikoani kwa ajili ya kutafuta wachezaji kuanzia umri wa miaka 5 hadi 16.
''Nimeamua kupumzisha kichwani changu, kwa kutulia katika soka la vijana kwa sababu mpira wetu unaongozwa na watu ambao hawana weledi hivyo naona nikianzia huku kwa vijana naamini siku za usoni Tanzania itakuja kuzalisha kina Clotaus Chama, Joash Onyago kwa kupitia vijana'' amesema Maxime.
Mkurugenzi wa Kituo hicho Zubeir Kambi ameeleza umuhimu wa kituo hicho katika soka la Tanzania ambapo pia makocha wengine wametambulishwa katika benchi hilo la ufundi ni pamoja na aliyewahi kuwa kocha wa magolikipa wa Simba Muharami Mohammed.
''Tumeamua kuwachukua makocha hao kutokana uzoefu waliona katika soka la Tanzania naamini ujio wao ndani ya kituo chetu utaleta matunda kwa soka la vijana '' amesema Mkurungenzi wa Cambiasso Sports Management Zubeir Kambi