Jumanne , 9th Jun , 2015

Mashindano ya Magari yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi siku ya Ijumaa Kisarawe mkoani Pwani, kwa kushirikisha madereva kutoka nchi za Uganda, Kenya na Zambia kama waalikwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa chama cha magari Tanzania Nizar Jivan amesema mashindano hayo yatakuwa ya siku ambapo yataanza Ijumaa hadi Iumapili na jumla ya magari 32 yatashiriki, ambapo yataanzia Tazara, kuelekea Kazimzumbwi, Banda Forest, Sungwi na kurudi Kazimzumbwe na Banda Forest.

Pia amesema mashindano yatazinduliwa na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi ambaye pia atafanyiwa hafla ya kumpongeza kutimiza umri wa miaka 90.

Naye Kamanda wa kikosi cha barabarani Mohamed Mpinga amesema watakuwa mkono kwa mkono katika kuimarisha usalama kwenye mashindano hayo.