Jumatano , 20th Jul , 2016

Mbeya City FC, wameomba mechi ya kirafiki na Mtibwa Sugar ikiwa ni maandalizi ya kupima kikosi chao kabla ya kuanza kwa msimu mwezi Agosti mwaka huu.

Siku kadhaa baada ya kuanza kwa kambi ya mazoezi kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya, tayari imethibitishwa kuwa kikosi  cha Mbeya City FC kitasafiri hadi mkoani Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Julai 30, mwaka huu.

Hii ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza mchezo wa kirafiki awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0 lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed  Ibrahim.

City  inatarajia  kuondoka  Mbeya  Julai  28 tayari  kwa mchezo huo  uliopangwa kupigwa  siku ya jumamosi ya mwisho wa mwezi huo.