Ijumaa , 5th Sep , 2014

Baada ya kucheza kwa mara ya kwanza katika uwanja wa taifa klabu ya soka ya Yanga ikiwa na kikosi kipya chini ya Mbrazil Marcio Maximo na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Thika United toka Kenya na timu kuonesha kiwango duni hatimaye

Kocha mkuu wa timu ya Yanga kushoto pichani Mbarazil Marcio Maximo.

Kocha Mkuu wa Dar es salaam Young Africans, Mbrazil Marcio Maximo amewaambia wanachama, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo, wawe wavumilivu na wawavutie subira wachezaji wapya waliosajiliwa ili wazoee na kuanza kufanya vitu vikubwa msimu huu

Akizungumza na Waandishi wa habari za michezo hii leo, makao makuu ya klabu, maeneo ya Jangwani, Dar es Salaam, Maximo amesema wachezaji wachezaji chipukizi na Wabrazil wenzake, kiungo Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’ wote ni wazuri

Maximo amesema ni mapema mno kuwatupia lawama wachezaji hao kwakuwa ni wachezaji wapya huku akisisitiza kuwa wabrazil wote ni wazuri, Coutinho na Jaja wataisaidia timu, mashabiki na wapenzi wawape muda, waache kuwazomea,

Maximo amesema ataaendelea kuwapa nafasi na anategemea wataonesha utofauti katika mchezo ujao wa kimaataifa wa kirafiki utakaopigwa siku ya Jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Bata Bullets ya Malawi,

Ambao Maximo amesema mchezo huo utakuwa wa mwisho kabla ya kumenyana na Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 14 mwaka huu

Tayari Yanga SC imekwisha cheza mechi nne za kujipima uwezo ikiwa chini ya Mabrazil Marcio Maximo tangu aanze kazi ya kukinoa kikosi hicho cha wanajangwani mwezi Julai na kushinda zote, imeshinda bao 1-0 mara mbili dhidi ya timu za Chipukizi ya Pemba na Thika United ya Kenya na 2-0 pia mara mbili dhidi ya Shangani na KMKM zote za Zanzibar, huku ikishuhudia wabrazil Andrey Coutinho na Genilson Santana Jaja kila mmoja akifanikiwa kufunga mabao mawili katika mechi hizo Nne walizoshuka dimbani kuichezea timu hiyo.