
Mshambuliaji Raphael Kiongera
Hanspoppe amesema, wameshafanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji ambao wanaamini watawasaidia katika kikosi hicho na kuweza kurekebisha matatizo yaliyokuwa ndani ya kikosi hicho kwa kuleta wachezaji watakaoongeza nguvu katika nafasi hiyo.
Hanspoppe amesema, kwa upande wa Mshambuliaji Mrundi Laudit Mavugo wapo katika mchakato wa kuwanaye na hapo awali sio kwamba walishindwa isipokuwa Mavugo alikuwa na mkataba na Rais wa timu ya Vital'o hivyo anamalizia mkataba na atakuwa mchezaji huru.
Hanspoppe amesema, pia wana mpango wa kumrudisha mshambuliaji Raphael Kiongera ambaye walimtoa kwa mkopo katika Klabu ya KCB ya nchini Kenya kwani ameonesha kurudi katika hali yake ya uchezaji.