Jumapili , 14th Jul , 2024

Timu ya Tanzania ya mchezo wa kikapu kwa vijana wenye umri chini ya miaka 16 imepoteza tena mchezo wa pili mbele ya Kenya katika michuano ya FIBA Africa U16 championship zone 5 inayoendelea katika viwanja vya shule ya Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani.

Tanzania imepoteza mchezo huo kwa vikapu 70 kwa 69 katika mchezo uliokuwa na kasi na vita nikuvute za hapa na pale.

Ikumbukwe hapo jana Tanzania ilipoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Burundi kwa vikapu 63 kwa 52.
-
Tanzania na Kenya zitacheza tena kesho ili kutafuta timu itakayocheza fainali ya michuano hiyo dhidi ya Burundi ambaye ameonekana kuwa mfupa mgumu kwa wavulana hao wa Tanzania na Kenya.