Kamishna wa ufundi wa shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania TBF, Manase Zabron amesema, walikuwa katika majadiliano ya wapi yafanyike mashindano hayo na wameshaafikiana kwa kuamua yafanyike Kibaha kutokana na kuwa na mahitaji yote muhimu ikiwemo viwanja vya michezo.
Zabron amesema, timu zitakazoshiriki mashindano hayo zinatakiwa kuanza maandalizi mapema ili kuleta ushindani katika mshindano hayo.
Zabron amesema mashindano hayo pia yatampa fursa kocha mkuu Methew Mc Colister kuangalia wachezaji na kuchagua watakaounda timu ya Taifa ambao watashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa pia yatamsaidia kuangalia mapungufu mbalimbali na changamoto za wachezaji.
Mashindano ya Taifa yanafanyika kila mwaka kwa kushirikisha timu mbalimbali kutoka katika mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani.



